Lugha Nyingine
Teknolojia ya kuonyesha za China zavutia umati katika Maonyesho ya CES 2025
Watu wakitembelea eneo la maonyesho la kampuni ya Hisense ya China kwenye Maonyesho ya Vifaa vya Kielektroniki vya matumizi (CES) 2025 mjini Las Vegas, Marekani, Januari 7, 2025. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)
LAS VEGAS, Marekani - Kwenye banda la Kampuni ya Hisense ya China katika Maonyesho ya vifaa vya matumizi vya Kielektroniki mwaka 2025 (CES), runinga kubwa inavutia watu huku ikionyesha Black Myth: Wukong, mchezo wa kompyuta unaotafutwa sana kwa mahitaji yake makubwa ya kuonyesha. Watembeleaji wa banda hilo wamekuwa wakisimama ili kutazama mchezo huo.
Joshua Liccardi, mchezaji wa michezo ya kompyuta kutoka Jimbo la Massachusetts la Marekani, amefurahishwa na hali halisi ya michezo huo wa kompyuta baada ya kuucheza kwa dakika takriban 10.
"Inapendeza kuonyeshwa kwenye skrini kubwa. Kiwango cha fremu ni kizuri sana. Inaonekana vizuri," amesema Liccardi, ambaye kwa kawaida hucheza michezo ya namna hiyo kwenye skrini za kompyuta.
"Pengine nitatafuta kitu kama hiki," ameongeza.
Watu wakitembelea eneo la maonyesho la kampuni ya TCL ya China kwenye Maonyesho ya Vifaa vya matumizi vya Kielektroniki (CES) 2025 mjini Las Vegas, Marekani, Januari 7, 2025. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)
Kauli hiyo imeungwa mkono na Dennys Li, Mkuu wa Kampuni ya Teknolojia ya kuonyesha ya Hisense. "Linapokuja suala la kuonyesha, watumiaji wanapendelea skrini kubwa kila wakati," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwenye maonyesho hayo CES 2025 yanayoendelea mjini Las Vegas.
Watu wakitembelea eneo la maonyesho la kampuni ya Changhong ya China kwenye Maonyesho ya Watumiaji wa Vifaa vya Kielektroniki (CES) 2025 mjini Las Vegas, Marekani, Januari 7, 2025. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)
Kwenye maonyesho hayo ya CES, bidhaa nyingine yenye uvumbuzi kutoka China zilizoundwa na kampuni kama vile TCL, BOE na Changhong zinavutia watu wengi pia, ikiwa ni pamoja na skrini ya kompyuta kwa ajili ya mchezo, skrini kwenye gari, projekta za kisasa na miwani ya AR.
Rob Rast, mbunifu maudhui ya dijitali kutoka California, amevutiwa hasa na kiigaji cha mashindano ya magari chenye skrini ya QD-Mini LED ya michezo ya kompyuta ya TCL .
"Ni safi sana. Ni furaha kuucheza na changamoto kuendesha," amesema Rast, akibainisha kuwa skrini iliyopinda inafanya uchezaji mchezo huo kuwa wa kihalisia zaidi -- "kama kuendesha gari halisi."
Katika banda la BOE, muundaji ongozi wa skrini nchini China, teknolojia za kisasa za chumba cha marubani zimepata ufuatiliaji mkubwa wa watu.
Skrini ya kielektroniki vimekuwa muhimu kwa uchumi, vikitumika kama sehemu muhimu yakuona na kugusa katika vifaa mbalimbali vya kielektroniki ya kutumiwa na walaji, kuanzia televisheni na kompyuta hadi vifaa vya mkononi, magari, vifaa tiba na vifaa vya nyumbani.
Roboti ya AI kutoka kampuni ya TCL ya China ikionyeshwa kwenye Maonyesho ya Vifaa vya Matumizi vya Kielektroniki (CES) 2025 mjini Las Vegas, Marekani, Januari 7, 2025. (Picha na Zeng Hui/Xinhua)
Teknolojia za kuonyesha za China zimekuwa zikichukua nafasi kubwa katika maonyesho hayo ya CES na katika soko la kimataifa katika miaka ya hivi karibuni.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma