China kuunganisha mipango ya maendeleo na Agenda ya Matumaini Mapya ya Nigeria: Wang Yi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2025

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Tuggar kwenye mkutano wao mjini Abuja, Nigeria, Januari 9, 2025. (Xinhua) /Yang Zhe)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi (kushoto), ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akipeana mkono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Yusuf Tuggar kwenye mkutano wao mjini Abuja, Nigeria, Januari 9, 2025. (Xinhua/Yang Zhe)

ABUJA - China inapenda kushirikiana na Nigeria kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mjini Beijing na kuendeleza mipango 10 ya utekelezaji wa ushirikiano nchini Nigeria, ikiandaa njia ya maendeleo mapya katika uhusiano wa pande mbili, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema mjini Abuja jana Alhamisi alipokutana na mwenzake wa Nigeria Yusuf Tuggar.

Nigeria, ikiwa ni nchi kubwa ya Afrika yenye ushawishi wa kimataifa na sehemu muhimu ya Nchi za Kusini, inatoa mchango usio na mbadala katika kutafuta amani na maendeleo barani Afrika, Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) amesema.

Wang amesema, China daima imekuwa ikitupilia macho maendeleo ya uhusiano wake na Nigeria kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu na inapenda kuimarisha mshikamano na ushirikiano na Nigeria, kuelewana na kuungana mkono katika masuala yanayohusu maslahi yao makuu, na kufikia kunufaishana katika michakato yao ya kujiendeleza na kustawisha.

Ameeleza kuwa, Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu alifanya ziara nchini China mwaka jana, ambapo wakuu wa nchi hizo mbili waliinua uhusiano wa pande mbili hadi kufikia ushirikiano wa kimkakati wa pande zote, wakikufungua matarajio mapya na mapana zaidi ya ushirikiano wa pande mbili.

“Chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu hao wawili, ushirikiano wa pande zote kati ya China na Nigeria umepata matokeo ya makubwa, ukileta manufaa halisi kwa watu wao,” ameongeza.

Amesema, China inapenda kuunganisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na mipango 10 ya utekelezaji wa ushirikiano na maeneo ya kipaumbele ya Ajenda ya Matumaini Mapya ya Nigeria kwa kutumia ushirikiano wa jadi katika miundombinu, kupanua ushirikiano wa kibiashara na mambo ya fedha, na kuanzisha mambo mapya katika ushirikiano wa uwekezaji ili kuimarisha zaidi uhusiano wenye matokeo halisi kati ya nchi hizo mbili.

Ametoa wito kwa Nigeria kulinda usalama na haki na maslahi halali ya kampuni na wafanyakazi wa China wanaofanya kazi nchini humo.

Kwa upande wake, Tuggar amesema Nigeria na China zina uhusiano mkubwa na wa muda mrefu, unaokita mizizi katika kuheshimiana na kuaminiana, hali ambayo imeleta mafanikio makubwa.

Nigeria na China hazina maoni ya tofauti na kuimarisha ushirikiano wao kunaendana na maslahi yao ya pande zote, amesema.

Tuggar amesisitiza Nigeria kushikilia bila kunyumbayumba kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuahidi kuendelea kuunga mkono msimamo wa China kwenye jukwaa la kimataifa, akibainisha kuwa ni jambo sahihi kufanya.

Pia ametoa salamu za rambirambi kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa unaojiendesha wa Xizang wa China, akipongeza juhudi za haraka na zenye ufanisi za serikali ya China katika kutoa misaada ya maafa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha