Umoja wa Mataifa wakadiria ukuaji wa uchumi duniani kuongezeka kwa asilimia 2.8 mwaka 2025

(CRI Online) Januari 10, 2025

Ripoti ya “Hali na Makadirio ya Uchumi Duniani Mwaka 2025” iliyotolewa jana Alhamisi na Umoja wa Mataifa imekadiria kuwa, ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka 2025 utaongezeka kwa asilimia 2.8, kiasi ambacho kinalingana na kile cha mwaka jana.

Ripoti hiyo imesema, ingawa uchumi wa dunia umeonesha ustahimilivu na kupitia changamoto mbalimbali, lakini bado uko chini ya asilimia 3.2, ambacho ni kiwango cha wastani kabla ya janga la COVID-19.

Ripoti hiyo pia imesema kupungua kwa mfumuko wa bei na sera za kuongeza mzunguko wa sarafu sokoni kunaweza kuchochea kwa kiasi ukuaji wa uchumi duniani. Hata hivyo, hali ya sintofahamu, migogoro ya siasa za kijiografia, na kuongezeka kwa mvutano wa kibiashara vitaleta hatari kubwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha