Moto wa nyika Kusini mwa California, Marekani walazimisha watu 180,000 kukimbia makazi yao

(CRI Online) Januari 10, 2025

Watu watano wamefariki na wakazi wapatao 180,000 kulazimika kukimbia makazi yao kutokana na moto wa nyika unaoendelea kuwaka kusambaa katika eneo la Los Angeles kusini mwa California nchini Marekani ukiteketeza maelfu ya majengo.

Kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni kutoka Idara ya Misitu na Udhibiti wa Moto ya California iliyotolewa Alhamisi asubuhi, kwa sasa kuna moto huo unasambaa katika sehemu tano, na jumla ya ukubwa wa eneo lililoteketezwa kwa moto linazidi kilomita za mraba 117.

Kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa, upepo mkali utashuhudiwa kwenye eneo hilo lenye kuwaka moto huo, huku kasi ya juu ya upepo huo ikikaribia kilomita 100 kwa saa.

Upepo mkavu na mkali, pamoja na mabadiliko katika mwelekeo wa upepo huo, vinaongeza hatari ya kusambaa zaidi kwa moto huo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha