Lugha Nyingine
Mji wa Kigali, Rwanda kutumia satalaiti kufuatilia kazi za ujenzi
Meya wa mji wa Kigali nchini Rwanda Bw. Samuel Dusengiyumva amesema mji huo unatazamiwa kutumia teknolojia inayowezeshwa na satalaiti kufuatilia ujenzi wa nyumba kwa lengo la kutambua shughuli za ujenzi holela ikiwa ni pamoja na vibali feki.
Bw. Dusengiyumva amewaambia wabunge wa Kamati ya Ardhi, Kilimo, Mifugo na Mazingira wa Bunge nchi hiyo kuwa wamepanga kutangaza kuanza matumizi ya teknolojia hiyo mpya siku chache zijazo.
Amesema mji wa Kigali utatumia teknolojia hiyo kwa ushirikiano na Shirika la Anga la Rwanda kutambua nyumba ambazo zimekuwa zinajengwa kila wiki, na kuzibomoa kabla hazijakamilika.
Amewaambia wabunge hao kuwa mfumo huo ulijaribiwa na kuonekana unafanya kazi vizuri. Ameongeza kuwa teknolojia hiyo imeunganishwa na mfumo wa kibali cha ujenzi na inaweza kuonyesha nyumba zinazojengwa bila vibali halisi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma