Lugha Nyingine
Afrika Kusini na Kenya miongoni mwa vyanzo vikuu vya utalii kwa Zanzibar kwa mwezi Desemba 2024
(CRI Online) Januari 10, 2025
Afrika Kusini na Kenya zimekuwa ni vyanzo muhimu vya watalii wanaotembelea visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania katika mwezi wa Desemba 2024, baada ya nchi hizo mbili kuibuka za pili na sita mtawalia, huku Italia ikishika nafasi ya kwanza.
Sekta ya utalii ya Zanzibar ilipata ongezeko kubwa katika mwezi Desemba, ikipokea wageni 91,611 wa kimataifa, ikiashiria ongezeko kubwa la asilimia 30.5 kutoka wageni 70,186 waliorekodiwa mwezi huo huo mwaka 2023.
Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar, zinaonesha kuwa Ulaya inaendelea kuwa chanzo kikuu cha watalii wa visiwa hivyo, ikichukua asilimia 68.1 ya watalii wote waliofika.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma