Watu 20 wauawa katika shambulio dhidi ya ikulu ya Chad

(CRI Online) Januari 10, 2025

Watu 20 wameuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya ikulu ya Chad lililotokea siku ya Jumatano jioni, taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini humo imesema.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, shambulio hilo lilitokea majira ya saa 1:45 jioni kwa saa za huko ambapo kundi la watu 24 wenye silaha walidai kuharibikiwa na gari na kushambulia walinzi katika mlango mkuu wa Ikulu.

Katika shambulio hilo, kundi hilo limeua askari wawili na kujeruhi vibaya askari wengine watano huku likijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya Ikulu.

Hata hivyo vikosi vya usalama vilijibu shambulio hilo haraka na kuua watu 18 kutoka kwenye kundi hilo, huku wengine 6 waliojeruhiwa wakikamatwa na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha