Mapigano yaliyotokea kaskazini mwa Syria yasababisha vifo vya watu zaidi ya 37

(CRI Online) Januari 10, 2025

Shirika la uchunguzi wa haki za binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza limesema mapigano makali yametokea kati ya vikosi vya wanamgambo wa kabila la Wakurdi vinavyoungwa mkono na Marekani na Jeshi la Syria linaloungwa mkono na Uturuki kwenye kitongoji cha Manbij, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 37 wakiwemo raia 5.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika hilo katika taarifa yake ya jana Alhamisi, watu 322 wakiwemo wapiganaji wenye sihala na raia wameuawa tangu mapigano hayo yalipotokea kwenye kitongoji hicho mwishoni mwa mwaka uliopita.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha