

Lugha Nyingine
Hakuna magonjwa mapya ya kuambukiza nchini China: China CDC
![]() |
Mkutano na waandishi wa habari ukifanywa na Kamisheni ya Kitaifa ya Afya ya China (NHC) mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 12, 2025. (Xinhua/Pan Xu) |
BEIJING - Hakuna magonjwa mapya ya kuambukiza nchini China, na magonjwa ya sasa ya kuambukiza ya kupumua nchini humo yote yanasababishwa na vimelea vinavyojulikana, Wang Liping, mtafiti katika Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha China (China CDC) amesema jana Jumapili, akibainisha kwamba mafua kwa sasa ndiyo ugonjwa unaosababisha watu wengi kwenda taasisi za afya kwa wagonjwa wenye maambukizi makali ya mfumo wa kupumua.
Takwimu zinaonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya mafua kinaendelea kuwa cha wastani katika mikoa mingi ya nchi hiyo, na wakati shule za msingi na za sekondari zinaingia likizo ya msimu wa baridi, kupungua kwa viwango vya maambukizi hayo ya mafua kunatarajiwa katikati mwa mwisho wa Januari, Wang amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Kamisheni ya Kitaifa ya Afya ya China (NHC).
Kuhusu maambukizi kwa binadamu ya kirusi cha metapneumo (HMPV), Wang amesema tayari yamekuwa yakisambaa kati ya binadamu kwa miongo kadhaa, na ongezeko la ripoti kuhusu maambukizi ya kirusi hicho katika miaka ya hivi karibuni inasababishwa na maendeleo ya njia za kupima na kubaini maambukizi.
Mtaalam huyo ameeleza kuwa, kiwango cha jumla cha magonjwa ya kuambukiza ya kupumua na shinikizo husika la matibabu mwaka huu halitazidi lile la mwaka jana.
“Licha ya ongezeko la watu kutembelea kliniki za homa na idara za dharura nchini kote China, idadi hiyo iko chini ya kiwango kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, na kumekuwa hakuna uhaba mkubwa wa rasilimali za matibabu,” amesema afisa wa NHC Gao Xinqiang.
“Tangu Oktoba 2024, kamisheni hiyo imekuwa ikifanya kazi na China CDC na mamlaka nyingine kuweka mipango na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara, kuhamasisha rasilimali na wafanyakazi kutoka kote nchini ili kuhakikisha kuwa huduma tiba zinaendelea kuwa thabiti na zenye utaratibu,” Gao amesema.
Kwa upande wa hatua za mwitikio wa mapema, Wang amesema matokeo ya uchunguzi wa mafua yanaonyesha kuwa aina kuu za maambukizi yanayozunguka kwa sasa miongoni mwa watu ni yale yanayosabaishwa na kirusi kidogo aina ya H1N1. Aidha, uchambuzi husika wa antijeni umethibitisha ufanisi wa chanjo ya mafua ya mwaka huu dhidi ya kirusi hicho.
“Uchambuzi husika wa uponyaji wa dawa pia unatoa mwelekeo kuwa virusi vya mafua vinayozunguka ni vyenye vihisi vikali kwa dawa za kuzuia virusi, ikithibitisha ufanisi wa matibabu ya dawa,” ameongeza.
Wang ameendelea kupendekeza kila mtu zaidi ya miezi sita anapokea chanjo ya mafua kila mwaka, mradi tu hakuna mikanganyiko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma