Ethiopia, Somalia zakubaliana kuboresha uhusiano kati yao baada ya mvutano wa hivi karibuni

(CRI Online) Januari 13, 2025

Ethiopia na Somalia zimekubaliana kurejesha na kuimarisha uhusiano ikiwa ni hatua muhimu kwa nchi hizo kupunguza mvutano wa kidiplomasia uliotokea hivi karibuni kati ya nchi hizo.

Makubaliano hayo yamefikiwa mjini Addis Ababa, kati ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ambaye alikuwa katika ziara ya kikazi nchini Ethiopia.

Viongozi wote wawili wamekubaliana "kurejesha na kuimarisha" uhusiano kati ya nchi zao kupitia uwakilishi kamili wa kidiplomasia katika miji yao mikuu.

Pia wamesisitiza ushirikiano wa karibu kati ya balozi zao katika masuala ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi kwa pande zote, na haja ya kuimarisha ushirikiano wa kiusalama, hasa katika kukabiliana na tishio linaloletwa na makundi ya wanamgambo wenye itikadi kali katika eneo lao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha