

Lugha Nyingine
Misri yapanua msukumo wa kidiplomasia wa Afrika huku msukosuko wa Bahari ya Sham ukiathiri uchumi
Misri inaongeza ushirikiano wa kidiplomasia na nchi za Afrika wakati inajaribu kuimarisha usalama katika eneo la kimkakati la Pembe ya Afrika na Bahari ya Sham, ambako migogoro inayoendelea imepunguza mapato yake kutoka kwenye mfereji wa Suez.
Juhudi hizo za kidiplomasia zinakuja wakati ambapo Misri inakabiliana na kupungua kwa asilimia 60 ya mapato yanayotokana na mfereji huo (dola za kimarekani karibu bilioni 7) katika kipindi cha miezi 11 iliyopita.
Rais wa nchi hiyo Abdel-Fattah al-Sisi amesema hasara hiyo imesababishwa na usumbufu dhidi ya meli kutokana na mashambulizi ya kundi la Houthi la Yemen kwenye Bahari ya Sham.
Mwishoni mwa wiki, siku ya Jumamosi Misri ilikuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa kamati mpya ya nchi tatu pamoja na Somalia na Eritrea, kufuatia mkutano wa kilele wa Oktoba kati ya viongozi wa nchi hizo nchini Eritrea.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma