

Lugha Nyingine
China na Ethiopia zaadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia
China na Ethiopia zimeadhimisha miaka 55 tangu kuanzishwa uhusiano wa kidiplomasia Jumapili mjini Addis Ababa.
Tukio hilo kubwa lililoandaliwa na Ubalozi wa China na Jumuiya ya Wafanyabiashara Wachina nchini Ethiopia, likiambatana na sherehe za sikukuu ijayo ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, lilikuwa na shughuli mbalimbali, ikiwemo mnada wa hisani, maonesho ya utamaduni wa China, vyakula vya jadi vya kichina na huduma bure za matibabu.
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China itaangukia Januari 29 mwaka huu, ikifungua Mwaka wa Nyoka, kwa mujibu wa kalenda ya kilimo ya China.
Akiongea katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na umati mkubwa wa Wachina na wenyeji, Balozi wa China nchini Ethiopia Bw. Chen Hai amesema, China itatumia maadhimisho hayo ya miaka 55 ya uhusiano kama mwanzo mpya, kutelekeza matokeo ya mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing na makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, na kufanya juhudi pamoja na marafiki wa Ethiopia kujenga mambo ya kisasa ya nchi hizo.
Akikumbusha kuwa China na Ethiopia zimeinua uhusiano wao hadi kufikia ngazi ya Uhusiano wa Washirika wa Kimkakati wa Pande Zote tangu mwezi Oktoba mwaka jana, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Mesganu Arga amesisitiza urafiki mkubwa kati ya China na Ethiopia, akisema kuwa uhusiano huo wa karibu ni ushahidi wa kile kinachoweza kufikiwa wakati mataifa hayo mawili yanaheshimiana na kutafuta maendeleo ya pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma