Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika yaimarisha urafiki wa siku zote: msemaji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2025

BEIJING – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiakun amesema ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika imepata mafanikio makubwa, kuimarisha urafiki wa siku zote kati ya China na Afrika na kuonyesha dhamira thabiti ya China na Afrika ya kuitikia kwa pamoja mabadiliko ya haraka katika dunia ya leo.

Ziara hiyo ya hivi karibuni ya Wang ilimfikisha katika nchi nne za Afrika, ambazo ni Namibia, Jamhuri ya Kongo, Chad na Nigeria. Ziara hiyo imeendeleza desturi ya miaka 35 ya mawaziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara Afrika katika ziara ya kwanza nje ya nchi kila mwanzoni mwa mwaka.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu, msemaji Guo ametoa maelezo zaidi juu ya ziara hiyo.

"Ziara hiyo imekamilika kwa mafanikio," Guo amesema, akiongeza kuwa mfululizo wa maafikiano na matokeo mapya yamepatikana katika utekelezaji wa mapendekezo sita na hatua 10 za ushirikiano zilizopendekezwa na Rais wa China kwenye Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2024.

Guo amesema kuwa hali ya kimataifa inabadilika kila wakati, lakini dhamira ya awali ya China na Afrika ya kutendeana kwa usawa na kuungana mkono ni thabiti kama mwamba.

Amesema, viongozi wa Afrika waliokutana na Waziri wa Mambo ya Nje Wang wamesisitiza tena dhamira yao ya kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja. Wameeleza kusikitishwa na tetemeko la ardhi katika Mkoa wa Xizang wa China.

Ameeleza kuwa, ziara hiyo imepata matokeo halisi, imehimiza ushirikiano kati ya China na Afrika katika nyanja mbalimbali, na kujenga maelewano mapana katika maeneo kama vile mawasiliano kati ya ustaarabu mbalimbali, maendeleo ya kijani na ushirikiano wa kilimo.

Aidha, amesema kuwa ziara hiyo pia imesaidia uratibu wa pande zote kati ya China na Afrika na juhudi kubwa za pamoja za kurekebisha dhuluma za kihistoria kwa Afrika, kuhimiza mshikamano na ustawi wa Nchi za Kusini na kujenga mfumo wa usimamizi wa kimataifa wenye haki na usawa.

"China na Afrika ziko mstari wa mbele katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu na zitakuwa mfano mzuri wa kuigwa katika jitihada hii," Guo amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha