Kituo cha anga ya juu cha China kufanya miradi zaidi ya 1,000 ya utafiti

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2025

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari za Anga ya Juu cha Beijing Novemba 16, 2024 ikionyesha chombo cha kubeba mizigo kwenda anga ya juu cha China, Tianzhou-8 wakati kikikamilisha kutua kwenye kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong kinachozunguka kwenye Orbit. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari za Anga ya Juu cha Beijing Novemba 16, 2024 ikionyesha chombo cha kubeba mizigo kwenda anga ya juu cha China, Tianzhou-8 wakati kikikamilisha kutua kwenye kituo cha anga ya juu cha China, Tiangong kinachozunguka kwenye obiti. (Picha na Han Qiyang/Xinhua)

SHANGHAI - Kituo cha anga ya juu cha China kitafanya miradi zaidi ya 1,000 ya utafiti, kuhimiza uenezi wa sayansi na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kipindi cha miaka 10 hadi 15 ijayo, kwa mujibu wa Kituo cha Teknolojia na Uhandisi cha Matumizi Kamilifu ya Anga ya Juu chini ya Akademia ya Sayansi ya China.

Kikifanya kazi kama maabara ya kitaifa ya anga ya juu, kituo hicho cha anga ya juu cha China kitapanga na kufanya ushirikiano wa kina wa utafiti mahsusi na wa taaluma mbalimbali katika muongo ujao, kikilenga kuleta mafanikio makubwa ya kisayansi na kiteknolojia na kuharakisha matumizi yake, Ba Jin, naibu mkurugenzi wa kitengo cha matumizi na maendeleo ya kituo hicho, amesema Jumatatu.

Katika nyanja ya sayansi ya maisha na utafiti wa binadamu katika anga ya juu, juhudi zitafanywa kuimarisha utafiti katika biolojia ya msingi, teknolojia ya kibaolojia na mabadiliko yake, ikolojia ya maisha, na asili ya maisha, ili kufichua zaidi mifumo ya athari na njia za mwitikio wa mazingira ya anga ya juu kwenye maisha.

“Katika nyanja ya sayansi ya fizikali ya mvutano ndogo, watafiti watafanya utafiti juu ya muundo na utaratibu wa udhibiti wa metali na aloi, ili kuelekeza utengenezaji wa nyenzo duniani” amesema Ba.

Watajaribu kuhimiza utatuzi wa muwako fanisi wa kaboni chache na kuongeza ufanisi wa mfumo wa umeme ili kutoa uungaji mkono kwa maendeleo ya umeme ya hali ya juu na nishati safi yenye ufanisi. Pia watachunguza mbinu mpya za kupozea atomiki na kujenga jukwaa changamano la majaribio ya plasma-fizikia.

Katika nyanja ya teknolojia mpya za anga ya juu na matumizi yake, lengo litakuwa kwenye mahitaji ya kimkakati ya kitaifa kama vile anga ya juu ya karibu ya Dunia na Dunia-Mwezi, na utafiti wa anga ya juu ya kina zaidi na huduma za obiti za siku zijazo.

Maendeleo yanatarajiwa kufanywa katika maeneo kama vile habari za anga ya juu na teknolojia ya upimaji sahihi, uundaji mambo katika obiti na teknolojia za ujenzi, na mifumo ya roboti na kiotomatiki.

Kwa mujibu wa Ba, miradi zaidi ya 80 ya kisayansi na matumizi imefanywa katika obiti, huku karibu tani mbili za nyenzo za kisayansi zikiwa zimewasilishwa na sampuli za majaribio aina karibu 100 zimerejeshwa duniani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha