Afisa Mwandamizi wa CPC akutana na wajumbe wa muungano wa vyama tawala vya Japan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 14, 2025

Li Shulei, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, akikutana na ujumbe wa muungano wa vyama tawala vya Japan, ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Liberal Democratic Hiroshi Moriyama na Katibu Mkuu wa Chama cha Komeito Makoto Nishida, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Januari 13, 2025. (Xinhua/Shen Hong)

BEIJING - Li Shulei, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC amekutana na ujumbe wa muungano wa vyama tawala vya Japan, ukiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Liberal Democratic Hiroshi Moriyama na Katibu Mkuu wa Chama cha Komeito Makoto Nishida, mjini Beijing.

Katika mazungumzo hayo Li ameukaribisha ujumbe huo wa Japan kufanya ziara nchini China kuhudhuria mkutano wa mazungumzo kati ya chama tawala cha China na Japan.

“Chama cha CPC kinapenda kushirikiana na muungano wa vyama tawala vya Japan ili kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kuimarisha mazungumzo ya kisiasa, kuhimiza mawasiliano kati ya watu na watu na kuweka mazingira mazuri ya maoni ya umma kwa ajili ya uhusiano kati ya China na Japan,” amesema Li.

Upande wa Japan umeeleza nia yake ya kutumia kikamilifu wajibu wa muungano huo wa vyama tawala kulingana na maafikiano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizo mbili, kukabiliana na matatizo na changamoto, na kuhimiza mawasiliano ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili, hususan mawasiliano ya vijana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha