

Lugha Nyingine
Afrika Kusini yateua waendeshaji biashara za utalii 65 kushughulikia viza kwa watalii wa China na India
Serikali ya Afrika Kusini imeteua waendeshaji biashara za utalii 65 watakaoshughulika na utoaji viza kwa watalii kutoka China na India.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afrika Kusini imetangaza kukamilika kwa mchakato huo wa kuteua kundi la kwanza la kampuni 65 za huduma za utalii kati ya kampuni zote 141 zilizowasilisha ombi la kujiunga na Mpango wa Waendeshaji Biashara za Utalii Wanaoaminika (TTOS), unaolenga kuvutia zaidi watalii kutoka China na India.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini Leon Schreiber amesema anatarajia kukaribisha ujio wa wimbi la kwanza la watalii chini ya mpango huo wa TTOS ndani ya wiki kadhaa, ikiwa ni hatua madhubuti ya kuonesha jinsi serikali ya awamu ya saba inavyofanya kazi pamoja kuleta mageuzi halisi na ukuaji wa uchumi ili kuongeza ajira.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma