Tanzania yazindua utalii wa nyuki katika nyanda za juu za kusini

(CRI Online) Januari 14, 2025

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) amezindua utalii unaohusiana na ufugaji nyuki katika wilaya ya Kalambo, mkoa wa Rukwa ulioko katika nyanda za juu za kusini za nchi hiyo, ili kuvutia watalii kwa shughuli za uzalishaji wa asali.

Ofisa mwandamizi wa TFS, Daniel Dotto amesema Serikali imeanzisha shamba na kusambaza mizinga 500 ya nyuki wilayani Kalambo ili kuendeleza utalii wa nyuki.

Ofisa mkuu wa uhifadhi wa TFS, Ibrahim Mkiwa amesema uzinduzi huo wa utalii wa nyuki ni sehemu ya juhudi za kuunga mkono Serikali katika kuongeza vivutio vya utalii.

Kwa mujibu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania, utalii unachangia asilimia 17.2 na asilimia 29 ya Pato la Ndani (GDP) la Tanzania na Zanzibar mtawalia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha