Shule ya Utawala ya Afrika yazinduliwa Rwanda

(CRI Online) Januari 15, 2025

Shule ya Utawala ya Afrika (ASG), ambayo ni taasisi ya kutoa kozi za shahada iliyosanifiwa kutoa programu za elimu za kiwango cha kimataifa katika taaluma za sera ya umma, utafiti, utawala, uongozi na usimamizi, imezinduliwa rasmi Jumanne mjini Kigali, Rwanda.

Ikiwa imeanzishwa kwa pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, kwa kushauriana na viongozi wengine wa Afrika, wasomi na wahisani, shule hiyo inalenga kutatua changamoto kubwa za kiutawala zinazolikabili Bara la Afrika kwa kuwezesha viongozi wanaoibuka kuwa na mawazo, uwezo na ujuzi hitajika kutekeleza uongozi wenye ufanisi kwa ajili ya siku zijazo za Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha