Kenya yalenga watalii wa mambo mapya 200,000 katika kipindi cha miaka mitano

(CRI Online) Januari 15, 2025

Wizara ya utalii ya Kenya imesema inalenga kuvutia watalii wanaotembelea na kujishughulisha na kufanya mambo mapya na yenye kutumikisha miili yao wapatao 200,000 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Waziri wa Utalii na Wanyamapori wa Kenya Bibi Rebecca Miano, amezindua Magical Kenya Mountain and Trail Series ili kupanua sekta hiyo mbali na fukwe na bidhaa za wanyamapori.

Waziri Miano amesema shughuli hiyo inajumuisha mambo mapya mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kupanda milima, kuendesha baiskeli, kujikita kwenye mambo ya kitamaduni, na kutembelea mashambani katika kaunti tano za Laikipia, Elgeyo Marakwet, Uasin Gishu, Baringo, na Nandi.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii ya Kenya June Chepkemei, amesema utalii wa aina hiyo utawezesha watalii kugundua mambo mapya yaliyofichika kwa kupita maeneo mbalimbali na kujionea tamaduni tajiri na tofauti za kaunti husika katika mpango huo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha