

Lugha Nyingine
Mauzo ya nje ya maua na mboga ya Kenya kwa mwaka 2024 yapungua hadi kufikia dola bilioni 1.06
Mapato ya kilimo cha bustani ya Kenya kwa mwaka 2024 yameshuka kutokana na kupunguzwa kwa usafirishaji hadi kwenye soko kuu la Ulaya na Asia.
Katibu Mkuu wa Idara ya Kilimo katika Wizara ya Kilimo na Mifugo ya Kenya Bw. Kipronoh Ronoh Paul, amesema Kenya ilipata dola za kimarekani bilioni 1.06 kutokana na mauzo ya bidhaa za bustani kwa mwaka 2024, ikiwa ni punguzo kutoka dola bilioni 1.21 zilizopatikana mwaka 2023.
Bw. Ronoh amesema kushuka huko kwa mapato kumetokana na kuimarika kwa shilingi ya Kenya, ambayo imefanya mauzo ya nje kuwa ghali zaidi na kupunguza mahitaji, pamoja na changamoto zinazotokana na ukosefu wa usalama katika Bahari ya Sham, hali ambayo imewalazimu wasafirishaji kutumia njia mbadala.
Mauzo makuu ya kilimo cha bustani nchini Kenya ni pamoja na mboga, matunda na maua, na soko kubwa zaidi ni Ulaya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma