

Lugha Nyingine
UNICEF yapokea msaada wa dola milioni 1.5 kwa ajili ya watoto wakimbizi wa Sudan nchini Libya
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limepokea ufadhili wa dola za kimarekani milioni 1.5 kutoka kwa Mfuko wa Elimu wa Umoja wa Mataifa Education Cannot Wait (ECW), kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya dharura ya kielimu na kisaikolojia ya watoto wakimbizi wa Sudan nchini Libya.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Libya, Mohammad Fayyazi amesema mchango huo kutoka mfuko wa ECW unawawezesha kuziba mapengo ya kielimu kwa watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Libya, na kuhakikisha hakuna mtoto hata mmoja anayeachwa nyuma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwakilishi huyo, programu hiyo inayolenga kufikia watoto elfu 19 kote nchini Libya, inatoa fursa rasmi na zisizo rasmi za elimu, ikihakikisha watoto wanaokumbwa na vizuizi kama vile ukosefu wa nyaraka za utambulisho, pia wanaweza kupata elimu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma