China yasema vikwazo, vizuizi na ukandamizaji wa Marekani havitazuia maendeleo yake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2025

BEIJING - Vikwazo, vizuizi na ukandamizaji wa serikali ya Biden havitazuia maendeleo ya China, Wizara ya Biashara ya China (MOC) imesema Jumatano, ikiongeza kuwa hata hivyo hatua hizo zitaimarisha tu imani na uwezo wa China katika kujitegemea na uvumbuzi wa kiteknolojia.

Wizara hiyo imesema, kwa kisingizio cha usalama wa taifa, serikali ya Biden imeongeza vizuizi vyake vya kibiashara dhidi ya China katika muda wake uliobakia madarakani. Hatua hizo ni pamoja na kuimarisha udhibiti wa usafirishaji nje wa teknolojia ya semiconductor na kudhibiti matumizi ya magari yenye kuungana na China, pamoja na programu na vifaa vyake nchini Marekani.

Serikali ya Biden imeanzisha ukaguzi wa usalama kwenye mifumo ya droni kutoka China na nchi zingine kuhusu teknolojia na huduma za habari na mawasiliano. Kampuni nyingi za China zimewekewa vikwazo, na mashirika mengi ya China yameongezwa kwenye orodha ya "masoko korofi", imeeleza wizara hiyo.

Wizara hiyo imesema, China imelalamika na inapinga vikali hatua hizo.

Imeeleza kuwa, hatua hizo za serikali ya Biden zimekiuka sana haki na maslahi halali ya kampuni za China, zikivuruga utaratibu wa soko na utaratibu wa biashara wa kimataifa. Imeongeza kuwa, hatua hizo zimeleta tishio kubwa kwa utulivu wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na usambazaji, ikisababisha madhara kwa biashara duniani kote, zikiwemo zile za Marekani.

“Kampuni nyingi kubwa na jumuiya za kiviwanda za Marekani zimepinga waziwazi baadhi ya hatua hizi, wakati nchi na kanda mbalimbali zimeonyesha kuchanganyikiwa na kutokubaliana,” wizara hiyo imesema.

“Hatua kama hizo ni mbinu wazi za kulazimisha na uonevu wa kiuchumi, ambazo hazina mantiki wala kuziwajibika. Zinadhuru si tu uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Marekani pekee lakini pia utulivu wa uchumi na maendeleo duniani,” wizara hiyo imesisitiza.

Wizara hiyo imeongeza kuwa, katika kukabiliana na vizuizi hivyo vya kibiashara vya serikali ya Biden, China itachukua hatua ili kulinda kithabiti mamlaka, usalama na maslahi yake ya maendeleo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha