

Lugha Nyingine
Simulizi ya Mhifadhi wa Wanyamapori Xinjiang: Kufuatilia vipepeo, kulinda mazingira ya asili ya eneo pori linalotelekeza la Xinjiang
Huang Yahui akipiga picha katika Milima ya Tianshan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini magharibi mwa China, mwaka 2024. (Xinhua)
URUMQI, Jan. 15 (Xinhua) -- Huang Yahui, mwenye umri wa miaka 40, amevutiwa na mazingira ya maumbile tangu utotoni. Alipokuwa na umri wa miaka zaidi ya 20 alishiriki katika shughuli za kijasiri na kujikita katika utafutaji wa ajabu kwenye mazingira ya asili.
Mwaka 2011, alipata fursa ya kubadilisha hali ya maisha, na kuwa mtu wa kujitolea katika timu ya utafiti iliyoongozwa na Ma Ming, profesa katika Idara ya utafiti wa Ikolojia na Jiografia ya Xinjiang ya Taasisi Kuu ya Sayansi ya China.
Uzoefu huo wa muda mfupi ulimsaidia katika kazi ya baadaye ya Huang, ambaye anaishi katika Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini magharibi mwa China.
Alikumbuka kuwa, "Wakati tai huyo mdhaifu wa kidhahabu aliyeinuliwa chini ya uangalizi wetu, akapanua mabawa yake na kuruka angani, nilihisi jukumu kubwa la kulinda mazingira ya kiikolojia ya maskani yangu na kujitolea kuhifadhi anuwai ya viumbe hai. "
Huang sasa ni mhifadhi wa muda wote wa wanyamapori na mwanzilishi mwenza wa kituo cha uhifadhi wa mazingira ya asili na uenezi wa ujuzi wa sayansi katika eneo la Saybag la mji mkuu wa Urumqi. Kituo hiki kinajikita katika kazi ya kuongeza uelewa wa kulinda mazingira ya asili na juhudi za kufanya uhifadhi.
Kuanzia Machi hadi Novemba kila mwaka, Huang na wenzake huishi na kufanya kazi nje, wakiwa na vifaa vya kupigia kambi, kamera, darubini na daftari. Wanapita kwenye misitu, milima na maeneo ya uwanda wa juu mkoani Xinjiang.
Amekuwa na shauku kubwa juu ya vipepeo, na katika muongo mmoja uliopita, amefanya kazi kwa bidii kurekodi hali ya sehemu waliko vipepeo na kutoa ripoti kuhusu uhifadhi wa ikolojia, na ameweka kumbukumbu za mamia ya spishi za vipepeo.
Katika zaidi ya miaka 10 iliyopita, Huang na wenzake wameweka kumbukumbu za zaidi ya spishi 200 za vipepeo na kuwasilisha matokeo yao ya utafiti kwa idara husika za misitu na mbuga na taasisi za utafiti, wakitoa takwimu muhimu kwa uhifadhi wa anuwai ya viumbe hai.
Picha hii ikionyesha Huang Yahui akiwa katika safari ya utafiti wa kisayansi katika Milima ya Tianshan, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini magharibi mwa China, mwaka 2015. (Xinhua)
Huang Yahui (Kulia) na mwenzake wakigundua mabaki ya wanyamapori waliokufa katika Milima Tianshan ya Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, kaskazini magharibi mwa China, mwaka 2018. (Xinhua).
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma