

Lugha Nyingine
Pande hasimu za Sudan Kusini kurejea kwenye mazungumzo nchini Kenya
Ujumbe wa serikali ya Sudan Kusini unatarajiwa kuwasili mjini Nairobi, Kenya Jumamosi wiki hii kurejea kwenye mazungumzo yanayolenga kutimiza amani na utulivu wa kudumu katika nchi hiyo changa zaidi duniani.
Yakiwa yamepewa jina la “Tumaini” mazungumzo hayo ya amani kati ya serikali ya mpito ya Sudan Kusini na makundi ya upinzani yamekuwa yakiendelea katika mji huo wa Nairobi tangu mwaka jana lakini yaliahirishwa ili kuruhusu mashauriano zaidi kati ya pande husika.
Mjumbe mkuu wa serikali ya Sudan katika mazungumzo hayo Bw. Kuol Manyang Juuk, ameeleza dhamira ya pande zote mbili kwa mazungumzo hayo yanayotarajiwa kuleta amani, utulivu na maafikiano nchini Sudan Kusini.
Mazungumzo hayo yanayoongozwa na Kenya ambayo yalianza Mei 9 mwaka 2024, yalikumbwa na changamoto mwezi Julai kufuatia pande kadhaa kueleza wasiwasi kuhusu taratibu mahsusi zilizopendekezwa katika majadiliano.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma