

Lugha Nyingine
Uganda katika hali ya tahadhari kufuatia mlipuko wa virusi vya Marburg nchini Tanzania
Uganda iko katika hali ya tahadhari kufuatia mlipuko unaoshukiwa kuwa ugonjwa wa Marburg (MVD) nchini Tanzania, ambao umesababisha vifo vya watu wanane.
Ofisa wa Wizara ya Afya ya Uganda amesema mamlaka ya afya imeongeza ufuatiliaji na kutekeleza hatua za tahadhari katika maeneo ya mpaka na Tanzania ili kuzuia virusi hivyo kuingia nchini Uganda.
Jumatatu wiki hii, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilizijulisha nchi wanachama kuhusu watu wanaoshukiwa kuambukizwa ugonjwa huo wa Marburg katika Mkoa wa Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania wakiwa na dalili za maumivu ya kichwa, homa kali, maumivu ya mgongo, kutapika na damu, udhaifu wa mwili na kutokwa damu.
WHO imesema tahadhari ya kikanda inachukuliwa kuwa ni kubwa, kutokana na umuhimu wa kimkakati wa Mkoa wa Kagera kama njia yenye pilika za watu wanaovuka mpaka kwenda Uganda, Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma