

Lugha Nyingine
Taasisi Kuu ya Sayansi ya China yawatunuku watangulizi wa ugunduzi katika sayansi na teknolojia
Chen Liquan kutoka Taasisi ya Fizikia katika Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS) akionekana kwenye picha mjini Beijing, China, Januari 15, 2025. (Xinhua/Jin Liwang)
BEIJING – Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS) imetangaza Tuzo ya Mafanikio Makubwa ya Sayansi na Teknolojia Mwaka 2024 jana Alhamisi, ikitambua wanasayansi wawili Chen Liquan kutoka Taasisi ya Fizikia katika CAS na Chen Xianhui kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha China ambao wametunukiwa Tuzo ya Mafanikio Binafsi na mafanikio mengine 14 ya kisayansi.
Chen Liquan, mwanataaluma wa Taasisi ya Uhandisi ya China, amejikita siku zote katika kufanya utafiti wa betri ya lithiamu kwa zaidi ya miaka 40 tangu mwaka 1976. Alianzisha nyanja ya ionics za hali-yabisi nchini China na akaongoza juhudi za mapema za China katika utafiti na maendeleo ya betri ya lithiamu. Mchango wake umeweka msingi na kutandika njia kwa ajili ya maendeleo ya siku hadi siku ya sekta ya betri ya lithiamu ya China.
Chen Xianhui, mwanataaluma wa CAS, amepiga hatua kubwa katika nyanja za mstari wa mbele za nyenzo za quantum, ikiwa ni pamoja na superconductors za Kagome, superconductivity ya kiolesura, na vizio vya topolojia vya sumaku. Kazi yake ya anzilishi imeweka msingi imara wa maendeleo ya kiteknolojia ya nyenzo za quantum, ikisukuma mbele maendeleo ya utafiti wa hali ya juu katika nyanja hiyo.
Miradi minne, ikiwa ni pamoja na utafiti kuhusu uundaji na mabadiliko ya awali ya Milky Way na mabadiliko ya aina mbalimbali ya mazingira ya Sayari Mirihi, imetunukiwa Tuzo ya Utafiti wa Msingi.
Tuzo ya Mafanikio Makubwa ya Sayansi na Teknolojia ya CAS, iliyoanzishwa mwaka 2002, inalenga kuwasifu watu binafsi au vikundi vya utafiti ambavyo vimetoa mchango mkubwa kwa ajili ya mafanikio makubwa ndani ya miaka mitano iliyopita. Uteuzi na uhakiki hufanywa kila baada ya miaka miwili.
Watafiti Du Aimin, Chen Ling, Qin Xiaoguang, Zhang Jinhai (kutoka kushoto hadi kulia) wa Taasisi ya Jiolojia na Jiofizikia katika Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS), wakionekana kwenye picha mjini Beijing, Januari 14, 2025. (Xinhua/Jin Liwang)
Mtafiti Chen Haisheng wa Taasisi ya Themofizikia ya Uhandisi katika Taasisi Kuu ya Sayansi ya China (CAS), akionekana kwenye picha mjini Beijing, Januari 14, 2025. (Xinhua/Jin Liwang)
Stempu za mwaka mpya wa nyoka zatolewa katika Taasisi ya Confucius mjini Minsk, Belarus
Mandhari ya Ziwa Sayram katika Mkoa wa Xinjiang, nchini China
Mahitaji ya dim sum na vitafunio yaongezeka nchini Indonesia kabla ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Michezo ya 32 ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani ya Majira ya Baridi yafunguliwa Turin, Italia
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma