Mjumbe Maalumu wa Rais Xi Jinping kushiriki hafla ya kuapishwa kwa rais mteule Trump

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2025

BEIJING – Kutokana na mwaliko wa upande wa Marekani, mjumbe maalum wa Rais Xi Jinping wa China, ambaye ni Makamu wa Rais wa China Han Zheng atakwenda Marekani kushiriki kwenye hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Marekani Donald Trump Januari 20 huko Washington, D.C., msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ametangaza leo Ijumaa.

Msemaji huyo amesema kuwa, siku zote China inafuata kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja katika kuzingatia na kukuza uhusiano kati ya China na Marekani.

"Tunapenda kuimarisha mazungumzo na mawasiliano na serikali mpya ya Marekani, kusimamia na kudhibiti migongano kwa mwafaka, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kufanya juhudi za pamoja za kuhimiza uhusiano kati ya China na Marekani uendelee na kupata maendeleo mazuri kwa hatua madhubuti na endelevu, na kutafuta njia moja ya kutendeana kwa usahihi kati ya nchi hizo mbili katika kipindi kipya,” msemaji huyo ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha