Ethiopia yawarejesha nyumbani raia wake 33,000 katika kipindi cha miezi 6

(CRI Online) Januari 17, 2025

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia imesema serikali ya nchi hiyo imewarejesha nyumbani raia takriban 33,000 waliokabiliwa na hali mbaya katika nchi za kigeni katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Nebiat Getachew, amesema juhudi kubwa zinazoendelea za kuwarejesha nyumbani watu hao ni sehemu ya dhamira ya kidiplomasia ya serikali ya Ethiopia ya “kuwajali raia” wake waliokwama katika hali ngumu na kuwarudisha nyumbani.

Msemaji huyo amefafanua juu ya baadhi ya raia waliorudishwa nyumbani kuwa ni pamoja na raia 380 waliotambuliwa kuwa katika hali mbaya nchini Myanmar. Watu hawa walipotoshwa na madalali walioahidi fursa za ajira, lakini baada ya kuwasili, walipelekwa kwenye kambi zisizoidhinishwa katika maeneo yanayopakana na Myanmar na Thailand.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha