

Lugha Nyingine
Balozi mpya wa China nchini Kenya asema China itafanya juhudi pamoja na Kenya kuimarisha ushirikiano
(CRI Online) Januari 17, 2025
Balozi mpya wa China nchini Kenya Bi. Guo Haiyan amesema China inapenda kushirikiana na Kenya katika kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.
Balozi Guo amesema hayo alimpomtembelea Mkuu wa Waziri wa Kenya ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Musalia Mudavadi, na kusema China na Kenya ni marafiki wenye historia ndefu, na China siku zote inatilia maanani uhusiano wake na Kenya.
Bw. Mudavadi amemkaribisha Balozi Guo na kusema uhusiano kati ya Kenya na China umeendelezwa vizuri, na miradi ya ushirikiano chini ya Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” imeimarisha uwezo wa kiuchumi wa Kenya na kuongeza ustawi wa watu wake.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma