Sudan Kusini, Benki ya Dunia zazindua mradi wa dola milioni 53 wa upatikanaji wa umeme

(CRI Online) Januari 17, 2025

Wizara ya Nishati na Mabwawa ya Sudan Kusini imezindua mradi wa nishati wa miaka mitano wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 53, unaolenga kuongeza upatikanaji wa huduma za umeme na kuimarisha uwezo wa kitaasisi katika sekta ya umeme.

Naibu katibu mkuu wa wizara hiyo, Sultan Lam Tungwar amesema, mradi huo uitwao ASSIST unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ni hatua muhimu ya kuongeza upatikanaji wa umeme, ambao ni kipengele cha kimsingi katika kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuboresha maisha ya watu.

Ofisa huyo amesema, ni asilimia 1 tu ya watu wa Sudan Kusini ndiyo wanapata huduma za umeme, ambazo pia ni za gharama kubwa, na mradi huo unatarajiwa kupanua upatikanaji wa huduma za umeme wa bei nafuu kwa watu na biashara nchini Sudan Kusini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha