Uchumi wa Kenya watarajiwa kukua kwa asilimia 5.3 mwaka huu

(CRI Online) Januari 17, 2025

Taarifa ya sera ya bajeti ya mwaka huu iliyotolewa mjini Nairobi na hazina ya Kenya, inaonesha kuwa uchumi wa Kenya kwa mwaka huu unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.3, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4.6 kutoka mwaka 2024, na asilimia 5.6 mwaka 2023.

Mwaka 2024 uchumi wa Kenya ulipungua kutokana na kudorora kwa shughuli za kiuchumi katika robo tatu ya kwanza ya mwaka, na kushuka kwa ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kwenye sekta muhimu.

Hazina pia imesema ukuaji wa mwaka huu utachochewa na tija ya kilimo iliyoimarishwa na sekta ya huduma himilivu.

Mahitaji ya ndani yanatarajiwa kuendelea kuwa himilivu, huku matumizi yakiwa na wastani wa asilimia 87.4 ya pato la taifa kwa mwaka huu, yakisaidiwa na kupungua kwa shinikizo la mfumuko wa bei.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha