Wataalam wahimiza uungwaji mkono wa kimataifa kwa juhudi za maendeleo ya kijani za Ethiopia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2025

Picha hii, iliyopigwa Februari 18, 2024, ikionyesha mandhari ya Bustani ya Urafiki mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

Picha hii, iliyopigwa Februari 18, 2024, ikionyesha mandhari ya Bustani ya Urafiki mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Li Yahui)

ADDIS ABABA - Wataalamu na watunga sera wamehimiza uungwaji mkono wa kimataifa kwa juhudi za Ethiopia katika kujenga uchumi wenye unyumbufu na wa kijani kama sehemu ya suluhu endelevu ya kukabiliana na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.

Haya yamekuja kwenye mkutano wa mwaka wa maendeleo wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) uliofanyika Ijumaa katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, wakati wataalam, watunga sera, na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wa maendeleo walipojadili juhudi za Ethiopia katika kujenga uwezo unaohimili mabadiliko ya tabia nchi na maendeleo endelevu.

Akihutubia mkutano huo, Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini Ethiopia, Samuel Doe amesema Ethiopia, ingawa inatoa kiasi kidogo cha gesi chafuzi, imeibuka kuwa "kiongozi asiye na kifani" katika kukabiliana na tishio lililopo la mabadiliko ya tabianchi na mtetezi mkubwa wa safari ya kijani ya Afrika.

"Tunaposimama kwenye hatari kubwa katika historia, tunafahamu kwa kina changamoto za kimataifa ambazo hazijawahi kutokea zinazoletwa na mabadiliko ya tabianchi. Changamoto hizi zinahitaji hatua za haraka, zinazoendeshwa na mshikamano wa dunia nzima, na matarajio ya pamoja ya mustakabali endelevu kwa wote," amesema.

Watu wakiwa wamepumzika kwenye Bustani ya Urafiki mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 18, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

Watu wakiwa wamepumzika kwenye Bustani ya Urafiki mjini Addis Ababa, Ethiopia, Februari 18, 2024. (Xinhua/Li Yahui)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha