Namibia yakaribisha nafasi ya 4 ya nchi zenye usalama zaidi barani Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 21, 2025

Picha hii, iliyopigwa Machi 25, 2024, ikionyesha mwonekano wa mtaa mjini Swakopmund, Namibia. (Xinhua/Chen Cheng)

Picha hii, iliyopigwa Machi 25, 2024, ikionyesha mwonekano wa mtaa mjini Swakopmund, Namibia. (Xinhua/Chen Cheng)

WINDHOEK - Wizara ya Mazingira, Misitu na Utalii ya Namibia (MEFT) imekaribisha orodha ya hivi karibuni ya Kampuni ya Usafiri wa Watalii ya Altezza, ambayo imeiweka Namibia kuwa nchi ya nne yenye usalama zaidi barani Afrika.

Utambuzi huo wa Altezza kwa usalama, utulivu wa kisiasa, na miundombinu ya utalii iliyoendelezwa ya Namibia ni mafanikio makubwa, msemaji wa MEFT Romeo Muyunda amesema katika taarifa yake, akiongeza kuwa nafasi hiyo siyo tu inaongeza hadhi ya nchi hiyo duniani bali pia inaimarisha nafasi ya Namibia ya sehemu muhimu ya kutalii.

Kwa mujibu wa Muunda, Namibia imeorodheshwa kwenye nafasi ya nne nyuma ya Mauritius katika nafasi ya kwanza, Ghana katika nafasi ya pili, na Zambia katika nafasi ya tatu.

"Nafasi hii inaonyesha asili ya amani ya sisi Wanamibia, lakini pia inasisitiza kwamba juhudi zetu za pamoja za kuhakikisha amani na utulivu zinatambuliwa. Wizara inawapongeza watu, vikundi vya usalama, vyombo vya usimamizi wa utekelezaji sheria, na wadau wote wa Namibia kwa kudumisha sheria na utulivu nchini,” ameongeza.

Watalii wakitazama wanyama sili wa Cape fur katika Hifadhi ya Cape Cross Seal, Namibia, tarehe 11 Oktoba 2023. (Xinhua/Chen Cheng)

Watalii wakitazama wanyama sili wa Cape fur katika Hifadhi ya Cape Cross Seal, Namibia, tarehe 11 Oktoba 2023. (Xinhua/Chen Cheng)

Msemaji huyo amesema kuwa ingawa Namibia imeorodheshwa kuwa ya nafasi ya nne, wizara hiyo inaamini kuwa nchi hiyo ina uwezo wa kuwa nchi salama zaidi barani Afrika.

Wakati huo huo, orodha hiyo ya nchi salama Afrika imekuja wakati kampeni inayoendelea ya usalama wa utalii inayoongozwa na wizara hiyo kwa ushirikiano na polisi, waendeshaji biashara ya utalii, na mabaraza ya kimikoa yaliyoteuliwa ya Namibia, miongoni mwa wadau wengine.

“Namibia ikiwa nchi moja ni lazima kutoa kipaumbele cha juu katika amani na utulivu kwani hali hiyo si tu itavutia watalii bali pia wawekezaji wanaohitajika sana ambao watahimiza maendeleo ya kiuchumi,” amesema.

Altezza, ambayo ni kampuni ya usimamizi wa maeneo ya kutembelewa na watalii yenye makao yake makuu mkoani Kilimanjaro, Tanzania, ilikusanya orodha hiyo ya viwango vya usalama wa nchi barani Afrika kwa kupitia utafiti mbalimbnali unaoongoza duniani katika miaka ya hivi karibuni, ukiwemo wa takwimu rasmi na maoni ya wananchi kuhusu usalama wa kibinafsi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha