"Mama" watatu wa Zhejiang na mtoto mmoja wa Xinjiang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2025

Saa 2 asubuhi Januari 15, 2025, katika wodi ya Hospitali ya Watoto yenye kumilikiwa na kuendeshwa na Shule ya Tiba ya Chuo Kikuu cha Zhejiang, China, mtoto mdodo wa kike mwenye umri wa miaka 7 wa Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang Mayire Ailisimu (baadaye tutamrejejelea kwa jina la Xiao Yiyi) anakaribia kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Katika siku 137 zilizopita alipotibiwa katika hospitali hiyo, Xiao Yiyi alikabiliana na changamoto mbalimbali na alikuwa na "mama" wengine watatu madaktari wa Zhejiang - Zhao Wenting, Yang Lijun na muuguzi mkuu Shan Jiani. Xiao Yiyi amezoea kuwaita Mama Zhao, Mama Yang na Mama Shan.

Xiao Yiyi akiinua uso wa Mama Zhao kabla ya kuagana kutoka hospitalini. (Picha na Chen Luxun/People’s Daily Online)

Xiao Yiyi akiinua uso wa Mama Zhao kabla ya kuagana kutoka hospitalini. (Picha na Chen Luxun/People’s Daily Online)

Mawasiliano ya mara kwa mara yaleta matumaini ya maisha

Yang Lijun ni msaidizi wa mkurugenzi wa Idara ya Kufeli kwa Moyo na Kusaidiwa na Mitambo katika Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang. Mwezi Mei 2024, alikwenda Xinjiang kutoa huduma za matibabu kwa bure na kutangaza shughuli ya ufadhili kwa kuokoa wagonjwa wenye matatizo ya kufeli kwa moyo.

Xiao Yiyi anatoka Wilaya ya Baicheng, Aksu, Xinjiang. Mwishoni mwa Juni 2024, alithibitishwa kuwa na ugonjwa wa moyo. Kwa pendekezo la daktari mwenyeji, alifika Hangzhou kwa ajili ya kupandikizwa moyo.

"Mtoto huyu alipoletwa hapa, tayari alikuwa katika hatua ya mwisho ya kufeli kwa moyo, na hali haikuwa na matumaini." Ili kutochelewesha matibabu yake, hospitali ilifungua njia ya haraka kwa Xiao Yiyi na kuita wataalam wote muhimu kwa mashauriano.

Hali ya Xiao Yiyi haikuwa na matumaini alipofika hospitalini. (Picha kwa hisani ya Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Hali ya Xiao Yiyi haikuwa na matumaini alipofika hospitalini. (Picha kwa hisani ya Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Septemba 13, Profesa Shu Qiang wa hospitali hiyo na timu yake walifanya upasuaji wa kupandikiza kifaa cha usaidizi cha watoto cha Jarvik2015 kwa Xiao Yiyi.

Ili kuwaondoa wasiwasi wazazi wa Xiao Yiyi, wafanyakazi wa matibabu walichangia kwa Xiao Yiyi na kutoa ombi ya pesa yuan laki 1.5 kutoka mfuko maalum kwa ajili yake. Mfuko wa Wanawake na Watoto wa Zhejiang ulianzisha akaunti kwa Xiao Yiyi, na mchango wa kijamii ulizidi yuan laki 8.2; wakati huo huo, hospitali hiyo iliwapatia makazi ya muda bila malipo na kuwasiliana na wafanyakazi wa kujitolea wanaozungumza lugha ya kiuyghur kuwasaidia kutatua tatizo la mawasiliano ya lugha, ili familia hiyo iwe na imani ya kutibu ugonjwa huo mjini Hangzhou.

Kutibu magonjwa na kutoa msaada wa kisaikolojia

Ili kumwezesha Xiao Yiyi kupona haraka iwezekanavyo, baada ya kujadiliana na wazazi wake, muuguzi mkuu Shan Jiani wa idara hiyo alianza kumfundisha mtoto huyo kula kwa kujitegemea, lakini hii si kazi rahisi. Kila siku kabla ya kula, Shan Jiani alikuwa akiongoza timu ya wauguzi kumpapasa Xiao Yiyi mgongoni, na kisha kutumia kifaa kumsaidia kufuta makohozi.

Xiao Yiyi, mama wake (katikati) na mama Shan (kulia) wakiwa wodini. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Xiao Yiyi, mama wake (katikati) na mama Shan (kulia) wakiwa wodini. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Si tu kufanya mazoezi ya kula, lakini pia mazoezi ya kutembea. Wakati wa ukaguzi wa kila siku, Zhao Wenting, ambaye anawajibika kwa usimamizi wa uimarishashi mwili baada ya upasuaji wa Xiao Yiyi, alikuwa akimtembeza.

Siku takriban 20 baada ya upasuaji, Xiao Yiyi alijaribu kutembea peke yake.Alipofanikiwa, alimwomba baba yake aende kwenye chumba cha zamu kumuita Zhao Wenting, isije akakosa kushuhudia hali hiyo .

"Mama Zhao, tazama, sikushikilia chochote!"

"Safi sana!"

"Hangzhou ni mji wetu wa pili"

Oktoba 11, 2024, akiwa ameambatana na "mama" watatu wa Zhejiang, Xiao Yiyi alisherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza umri wa miaka 7 hospitalini hapo siku moja mapema.

Xiao Yiyi akila keki ya siku ya kuzaliwa. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Xiao Yiyi akila keki ya siku ya kuzaliwa. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Desemba 2, mtoto Yiyi alipata moyo wa kupandikizwa, upasuaji wa upandikizaji wa moyo ulifanikiwa sana.

Baada ya majira ya baridi, mtoto Yiyi, ambaye sasa anaweza kutembea kwa kujitegemea, anaenda kwenye chumba cha zamu na kituo cha wauguzi ili kuonana na "mama".

Baada ya utunzaji mzuri, hali ya Xiao Yiyi imekuwa bora zaidi siku hadi siku. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

Baada ya utunzaji mzuri, hali ya Xiao Yiyi imekuwa bora zaidi siku hadi siku. (Picha imetolewa na Hospitali ya Watoto ya Chuo Kikuu cha Zhejiang)

"Xinjiang ni nyumbani kwetu, na Hangzhou ni mji wa pili wa nyumbani kwetu." Baba wa Xiao Yiyi Alisim Wusman ametoa shukrani, "Serikali na hospitali hapa imetupatia urahisi katika pande zote, asanteni sana!"

Kaka wa Xiao Yiyi Abdusalam Ai'erxi pia alikwenda nyumbani kwa ajili ya likizo, na familia hiyo ya watu wanne hatimaye imejumuika pamoja tena: "Kushuhudia dada yangu mdogo akirudi salama, ninawashukuru hasa wale wote waliosaidia familia yetu."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha