China yaongeza nafasi mpya za ajira milioni 12.56 mijini mwaka 2024, hali ya ajira yawa shwari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2025

Watafuta kazi wakizungumza na waajiri kwenye maonyesho ya nafasi za ajira yaliyoandaliwa kwa wahitimu wa Mwaka 2025 wa Chuo Kikuu cha Heilongjiang mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Desemba 23, 2024. (Xinhua/Zhang Tao)

Watafuta kazi wakizungumza na waajiri kwenye maonyesho ya nafasi za ajira yaliyoandaliwa kwa wahitimu wa Mwaka 2025 wa Chuo Kikuu cha Heilongjiang mjini Harbin, Mkoa wa Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China, Desemba 23, 2024. (Xinhua/Zhang Tao)

BEIJING – Wizara ya Uajiri na Uhakikisho wa Kijamii ya China imetangaza jana Jumanne kuwa, nafasi mpya za ajira milioni 12.56 zimetolewa mijini China katika mwaka 2024 uliopita, ikifikia lengo la mwaka.

Mwaka 2024, kiasi cha ukosefu wa nafasi za ajira mijini nchini China kilifikia asilimia 5.1, ikiwa ni asilimia 0.1 chini ya mwaka uliopita, wizara hiyo imeeleza.

Nchi hiyo ilikuwa imeweka lengo la mwaka la la kutoa nafasi mpya za ajira zaidi ya milioni 12 mijini mwaka 2024 na pia ililenga kuweka kiasi cha watu wasio na kazi kilichofanyiwa uchunguzi kuwa karibu asilimia 5.5 kwa mwaka.

"Hali ya kupata nafasi za ajira imeendelea kuwa tulivu kwa ujumla," amesema Lu Aihong, msemaji wa Wizara ya Uajiti na Uhakikisho wa Kijamii ya China kwenye mkutano na waandishi wa habari.

“Kufikia mwisho wa mwaka 2024, watu zaidi ya milioni 33.05 walioondokana na umaskini wameajiriwa,” Lu amesema.

Msemaji huyo amesema, wamiliki wa kadi za uhakikisho wa kijamii nchini China walifikia bilioni karibu 1.39 kufikia mwisho wa mwaka jana, ikiwa ni pamoja na watumiaji wa kadi za kidijitali bilioni 1.07.

Kadi za uhakikisho wa kijamii zimegawanywa katika kadi halisi na kadi za kidijitali. Watu wengi wanamiliki aina zote mbili.

Lu amesema kuwa wizara hiyo pia imeimarisha usimamizi sanifu wa tathmini ya uwezo wa kazi za ufundi, ambapo watu zaidi ya milioni 12 wamepata vyeti vya kiwango cha kazi za ufundi au vyeti vya kufuzu kwa taaluma mwaka jana.

Wizara hiyo imetangaza kuwa mwaka 2025, programu lengwa ya kuunga mkono ajira kwa sekta, viwanda, mashina ya mijini hadi vijijini, pamoja na biashara ndogo zaidi, ndogo na za kati zilizo muhimu itatekelezwa, ikianzisha utaratibu wa kukusanya na kutoa taarifa za nafasi za kazi zinazohusiana na miradi mikubwa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha