

Lugha Nyingine
China na AU zasherehekea mafanikio katika uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi
ADDIS ABABA - China na Afrika zimefurahia mafanikio makubwa katika uhusiano wao wa kidiplomasia na kiuchumi huku kukiwa na kuzidishwa kwa ushirikiano katika masuala ya kimataifa na kikanda, maafisa wa China na Umoja wa Afrika (AU) wamesema Jumatatu katika jengo jipya la Ujumbe wa China kwenye AU mjini Addis Ababa, Ethiopia, wakati wa hafla ya kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China itaangukia Januari 29 mwaka huu, ikikaribisha Mwaka wa Nyoka, kulingana na kalenda ya kilimo ya China.
Hu Changchun, mkuu wa ujumbe wa China kwenye Umoja wa Afrika, amesema kwenye hafla hiyo kuwa uhusiano kati ya China na Afrika umeinuliwa na kuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote kwa zama mpya.
"Haijalishi jinsi hali ya kimataifa na kikanda inavyobadilika, China siku zote ni rafiki wa kutegemewa wa Afrika, mshirika wa uhakika zaidi katika kutafuta maendeleo ya Afrika, na muungaji mkono mkubwa wa Afrika katika jukwa la kimataifa," amesema.
Amesema, Serikali ya China imedhamira kushirikiana na marafiki wa Afrika ili kutekeleza matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kutekeleza "hatua 10 za ushirikiano," na kufanya kazi pamoja katika njia ya kuelekea ujenzi wa mambo ya kisasa.
Monique Nsanzabaganwa, naibu mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, amesema ushirikiano kati ya AU na China umepata matokeo mazuri na yenye matunda katika miaka iliyopita, akibainisha desturi ya waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara barani Afrika katika ziara zao za kwanza za nje ya nchi kila mwanzoni mwa mwaka kwa miaka 35 iliyopita.
"Katika miaka ya hivi karibuni, kuaminiana kisiasa kati ya Umoja wa Afrika na China kumeendelea kuimarika, na pande hizo mbili zimeshirikiana kwa karibu katika masuala ya kimataifa na kikanda," Nsanzabaganwa amesema.
Kwa mujibu wa Nsanzabaganwa, mwaka 2025 ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa Kilele wa Beijing wa FOCAC Mwaka 2024, na AU inapenda kuimarisha ushirikiano wa kina wa mikakati ya maendeleo na China na kuweka mfano wa ushirikiano wa kimataifa kwa pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma