

Lugha Nyingine
Ramani ya Kiingereza ya Mji wa Beijing, China yatolewa kwa utumiaji wa majaribio
Picha hii iliyopigwa Agosti 12, 2024 ikionyesha Jengo la Ngoma linaloonekana kutoka Kilima cha Jingshan kwenye njia ya mstari wa katikati ya Beijing siku ya jua kali mjini Beijing, China. (Xinhua/Li Xin)
BEIJING - Hivi karibuni mji wa Beijing wa China umetoa ramani ya Kiingereza ili kuimarisha huduma za usafiri kwa raia wa kigeni katika mji huo ambapo ramani hiyo sasa inapatikana kwa utumiaji wa majaribio wa mwezi mmoja kwenye Jukwaa la Beijing la Huduma za Taarifa za Pamoja za Kijiografia.
Ramani ya Kiingereza ya Beijing ina toleo la kidijitali na ya kuchapishwa. Ramani ya kidijitali inahusisha mgawanyo wa maeneo ya mambo ya utawala, maeneo ya mazingira ya asili, usafiri, taasisi za serikali, mashirika ya kimataifa, elimu na utamaduni, matibabu na afya, michezo na burudani, maeneo ya makazi na majengo ya biashara, ikiwa na maelezo zaidi ya 30,000 kwa jumla.
Ramani ya kidijitali inahusisha mada sita zenye maelezo zaidi ya 4,000, kama vile huduma za kadi za benki na huduma za SIM kadi, zikitoa taarifa rahisi kwa wageni wanaotembelea, kuwapa urahisi katika kazi na maisha yao Beijing.
Ramani iliyochapishwa inaonesha hasa alama za maeneo ya kihistoria kama vile njia ya mstari wa katikati ya Beijing. Toleo la kidijitali la ramani hiyo linaweza kupatikana bila malipo kwenye tovuti ya Ramani ya Dunia.
Wakati wa utumiaji wa majaribio, maoni yatakusanywa ili kuboresha na kuongeza mambo ya ramani hiyo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma