

Lugha Nyingine
China yatangaza hatua za kupanua ufunguaji mlango wa mambo ya kifedha
Picha hii ya angani iliyopigwa Septemba 10, 2023 ikionyesha mwonekano wa eneo la Zhangjiang la Eneo la Majaribio ya Biashara Huria la China (Shanghai) mjini Shanghai, mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
BEIJING - China imetangaza mwongozo, unaoelezea hatua 20 za kupanua ufunguaji mlango wa mambo ya kifedha katika maeneo ya majaribio ya biashara huria na bandari ya biashara huria ya nchi hiyo.
“Hatua hizi, zinazojikita katika maeneo sita, zinalenga kuwianisha vyema sekta ya fedha ya China na viwango vya kimataifa na kuendeleza ufunguaji mlango wa kitaasisi wa sekta hiyo,” unasema mwongozo huo uliotolewa kwa pamoja na Benki Kuu ya China, Wizara ya Biashara ya China na vyombo vingine vitatu vya serikali.
Kwa mujibu wa waraka huo, taasisi za kifedha za kigeni zitapewa huduma sawa na wenzao wa China wakati zikitoa huduma mpya za mambo ya kifedha ambazo hazipatikani nchini katika kipindi hicho.
Maombi halali yaliyowasilishwa na taasisi za kifedha na watoa huduma za kuvuka mpaka za mambo ya kifedha yanayohusu huduma za mambo ya fedha yatashughulikiwa ndani ya siku 120, mwongozo huo umeeleza.
“China pia itaunga mkono ununuzi wa aina fulani za huduma za kuvuka mipaka za mambo ya kifedha, kuwezesha uhamishaji wa fedha zinazoingia na kutoka nje zinazohusiana na uwekezaji wa kigeni, kuboresha mipangilio ya mtiririko wa kuvuka mpaka wa data za mambo ya kifedha, na kuimarisha udhibiti wa sekta hii”, mwongozo huo unasema.
Mwongozo huo umefafanua kwamba, hatua hizo zitatekelezwa katika maeneo ya majaribio ya biashara huria mjini Shanghai, Guangdong, Tianjin, Fujian na Beijing, pamoja na Bandari ya Biashara Huria ya Hainan na majukwaa mengine muhimu ya ushirika.
Kwenye Mkutano wa Kamati Kuu ya Kazi ya Uchumi ya China uliofanyika mwezi uliopita, watunga sera wa China walisisitiza haja ya kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu na kuweka biashara ya nje na uwekezaji wa kigeni katika hali tulivu.
Mkutano huo ulieleza kuwa, China itaongeza kwa kasi tulivu ufunguaji mlango wa kitaasisi na kuboresha ubora na ufanisi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma