

Lugha Nyingine
Semina ya mwelekeo wa kimataifa wa uvumbuzi wa elimu ya ufundi stadi yafanyika
BEIJING - Semina ya mwelekeo wa kimataifa wa uvumbuzi wa elimu ya ufundi stadi iliyoandaliwa na Taasisi ya Elimu ya Sayansi ya China na Tovuti ya Gazeti la Umma(People’s Daily Online) imefanyika Januari 20 mjini Beijing.
Semina hiyo iliyofanyika chini ya kaulimbiu ya “Mwelekeo wa Kimataifa wa Uvumbuzi wa Elimu ya Ufundi Stadi”, imefanyika mtandaoni na ana kwa ana ukumbini, ikihudhuriwa na wajumbe na washiriki zaidi ya 200 kutoka idara za serikali, mashirika ya kimataifa, vyuo vikuu vya kawaida, kampuni na taasisi mbalimbali.
Washiriki wamejadili kwa pamoja kuhusu hali ya maendeleo ya elimu ya ufundi stadi, huku wakifanya mawasisho ya kina kuhusu mwelekeo wa kimataifa wa elimu ya ufundi stadi.
Katika semina hiyo, taasisi ya elimu ya sayansi ya China imetoa ripoti kuhusu “Mwelekeo wa Kimataifa wa Uvumbuzi wa Elimu ya Ufundi Stadi 2025” ambapo ripoti hiyo inaonesha kuwa mwelekeo wa kimataifa wa uvumbuzi wa elimu ya ufundi stadi imeangazia mambo kadhaa.
Mambo hayo ni pamoja na bidhaa za umma, ambapo inaonesha sifa ya bidhaa za umma siku hadi siku. Jambo la pili, ni ufundi wa jumla, kuanzia kuzingatia upande mmoja hadi kujiendeleza kwa ujumla na jambo la tatu, ni uratibu wa pande nyingi kwa kuzingatia uratibu wa pande tofauti na ugavi anuai.
Aidha mambo mengine yaliyoainishwa na ripoti hiyo ni pamoja na mabadiliko ya kidijitali, mafunzo ya maisha yote, mfumo wa mwalimu mwenye uwezo wa mhandisi, utaratibu wa kisheria, ujumuishaji wa kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma