

Lugha Nyingine
Taasisi ya Confucius kuanza kozi ya lugha ya Kichina katika shule ya sekondari ya Botswana
Hafla ya kutia saini Mkataba wa Makubaliano ikifanyika Gaborone, Botswana, Januari 23, 2025. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
GABORONE - Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Botswana (CIUB) imetia saini Mkataba wa Maelewano (MoU) na Chuo cha Livingstone Kolobeng (LKC) siku ya Alhamisi kutambulisha Lugha ya Kichina kama lugha ya pili kufundishwa katika shule ya sekondari.
Kutokana na ushirikiano huo, LKC inakuwa shule ya kwanza ya sekondari ya Botswana kutoa kozi ya lugha ya Kichina kama sehemu ya mtaala wa mtihani wa Cambridge.
Akizungumza kwenye hafla ya utiaji saini makubaliano hayo mjini Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Mkuu wa LKC Jeff Ramsay amepongeza makubaliano hayo kama hatua muhimu kuelekea lengo la shule hiyo la kuwa kiongozi duniani katika elimu ya kimataifa.
"Mpango huu unasaidia kuimarisha maisha ya kiweledi, maendeleo ya kitamaduni, na mchango katika kuongeza uelewa wa kitaaluma na ushirikiano kati ya taasisi mbili za elimu," Ramsay amesema.
Ameongeza kuwa, mpango huo unalenga kuimarisha mtaala wa kimataifa, kuhimiza maelewano, na kuongeza ufahamu wa kitamaduni wa wanafunzi, ikiwatayarisha kwa fursa na taaluma za kimataifa, haswa nchini China.
Pu Durong, mkurugenzi wa China wa CIUB, amebainisha kuwa mpango huo utanufaisha taasisi zote mbili na kuigeuza LKC kuwa shule bora yenye sifa za kufundisha lugha ya Kichina, ikiifanya kuvutia zaidi kwa wanafunzi na wazazi.
Amesisitiza kuwa wanafunzi pia watapata fursa ya kushiriki katika mashindano ya mwaka ya daraja la Lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa shule za sekondari, ambapo wanaweza kushindana kimataifa katika lugha na utamaduni wa Kichina.
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma