Rais Xi Jinping atoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wote

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2025

Picha hii ya kuunganishwa ikimuonesha Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza kwa njia ya video na  wajumbe wa wanajeshi kutoka majeshi yote ya China, Januari 24, 2025. (Xinhua/Li Genge)

Picha hii ya kuunganishwa ikimuonesha Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akizungumza kwa njia ya video na wajumbe wa wanajeshi kutoka majeshi yote ya China, Januari 24, 2025. (Xinhua/Li Genge)

SHENYANG – Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ametoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wanajeshi wote wa China kwenye ziara yake ya ukaguzi katika ofisi za eneo la kivita la kaskazini siku ya Ijumaa.

Rais Xi, akiwa kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama na Kamati Kuu ya Kijeshi ametoa salamu za dhati kwa askari wa PLA na Jeshi la Polisi la Umma la China, watumishi wa ofisini katika jeshi, na wanamgambo na wale wa vikosi vya akiba.

Tarehe 29 Januari itakuwa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, kwa kalenda ya kilimo ya China.

Siku ya Ijumaa asubuhi, Rais Xi alikutana na maofisa na askari wa eneo la kivita la kaskazini PLA. Kisha amezungumza kwa njia ya video na wajumbe wa wanajeshi kutoka majeshi mbalimbali ya China.

Maofisa na askari hao wa majeshi mbalimbali ya China walimwelezea Rais Xi juu ya majukumu yao ya utayari wa kupigana vita na hali ya utekelezaji wa majukumu. Rais Xi amepongeza sana kazi yao.

Amesema wanajeshi wanapaswa kuimarisha utekelezaji wa majukumu yao ya utayari wa kupigana vita ili kukabiliana kwa ufanisi na dharura yoyote na kulinda usalama wa nchi na utulivu wa jamii wakati wa likizo hiyo.

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa na askari wa  eneo la kivita la  kaskazini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Januari 24, 2025 (Xinhua/Li Genge la Li)

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), akiwa katika picha ya pamoja na maofisa na askari wa eneo la kivita la kaskazini la Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA), Januari 24, 2025. (Xinhua/Li Genge la Li)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha