China yawa soko kubwa zaidi la mauzo ya bidhaa za rejareja mtandaoni kwa miaka 12 mfululizo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2025

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China ilifanya Mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing kuhusu kuhakikisha utoaji wa bidhaa sokoni na uhimizaji wa matumizi ya manunuzi wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China  Januari 24, 2025. (Xinhua/Pan Xu)

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China ilifanya Mkutano na waandishi wa habari mjini Beijing kuhusu kuhakikisha utoaji wa bidhaa sokoni na uhimizaji wa matumizi ya manunuzi wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China Januari 24, 2025. (Xinhua/Pan Xu)

BEIJING - China imekuwa soko kubwa zaidi la mauzo ya bidhaa za rejareja mtandaoni kwa miaka 12 mfululizo, huku mauzo ya rejareja mtandaoni yakifikia thamani ya yuan trilioni 15.5 (dola za Kimarekani kama trilioni 2.16) mwaka 2024, Wizara ya Biashara ya China imetangaza.

“Tasnia za uuzaji bidhaa kwa bei ya jumla na rejareja za China zimepata maendeleo tulivu chini ya uhimizaji wa sera mbalimbali, zikitoa uungaji mkono mkubwa kwa ajili ya kupanua mahitaji ya ndani na kuanzisha muundo mpya wa maendeleo,” Naibu Waziri wa Biashara wa China Sheng Qiuping ameuambia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku ya Ijumaa.

Sheng amesema kuwa thamani iliyoongezwa ya tasnia za mauzo ya jumla na ya rejareja ilifikia yuan trilioni 13.8 mwaka 2024, ikichukua asilimia 10.2 ya Pato la Taifa la China na kutoa mchango muhimu katika kulainisha mzunguko, kuongeza nafasi za ajira na kupunguza gharama za uchukuzi na usambazaji.

Ameongeza kuwa, wizara hiyo itashirikiana na idara husika ili kuimarisha zaidi sera za ungaji mkono, kutekeleza hatua halisi na kuharakisha uhimizaji wa maendeleo ya sifa bora ya tasnia za mauzo ya jumla na ya rejareja, ili kuboresha zaidi mzunguko wa uchumi wa taifa. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha