China na Marekani zinapaswa kutafuta njia sahihi ya kuendana pamoja katika zama mpya: Wang Yi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 26, 2025

BEIJING - China na Marekani zinapaswa kutafuta njia sahihi ya kuendana pamoja katika zama mpya, Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio kwa njia ya simu yaliyofanyika kutokana na mwaliko wa Rubio siku ya Ijumaa.

Wang, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema Rais Xi Jinping wa China alifanya mazungumzo muhimu na Rais wa Marekani Donald Trump kwa njia ya simu Ijumaa wiki mbili zilizopita na kufikia makubaliano mbalimbali na kwamba maendeleo ya uhusiano kati ya China na Marekani yameingia katika hatua mpya muhimu.

"Rais Xi alifafanua kwa kina sera ya China kwa Marekani, na Trump alijibu vyema, akielezea matarajio yake ya kudumisha uhusiano mzuri na Rais Xi na kusisitiza kuwa ushirikiano kati ya Marekani na China unaweza kutatua matatizo mengi duniani," Wang amesema.

Wakuu hao wawili wa nchi walielezea mwelekeo na kuweka mmsingi wa uhusiano kati ya China na Marekani, Wang amesema, akiongeza kuwa timu za pande zote mbili zinapaswa kufuata makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu hao wa nchi, kudumisha mawasiliano, kusimamia tofauti, kupanua ushirikiano kwa kutilia maanani kanuni za kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wa kunufaishana.

Wang amesema kuwa kuongozwa na CPC ni chaguo la watu wa China na kwamba maendeleo ya China yana mantiki dhahiri ya kihistoria na nguvu kubwa endeshi ya ndani, akiongeza lengo la China ni kutoa maisha bora kwa watu na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa dunia.

Akifafanua juu ya kanuni na msimamo wa China kuhusu suala la Taiwan, Wang ameitaka Marekani ishughulikie kwa tahadhari akisema kuwa, Taiwan imekuwa sehemu isiyotengeka ya China tangu enzi za kale.

"China haitaruhusu kamwe Taiwan kutengwa na nchi mama," amesisitiza.

Kwa upande wake Rubio amesema kuwa Marekani na China ni nchi mbili kubwa na kwamba uhusiano kati ya Marekani na China ni uhusiano muhimu zaidi wa pande mbili katika karne ya 21 na utatengeneza mustakabali wa siku za baadaye wa dunia.

Amesema Marekani ina nia ya kufanya mawasiliano na China kwa wazi, kutatua tofauti ipasavyo, kusimamia uhusiano wa pande mbili kwa njia iliyokomaa na ya tahadhari, kushughulikia kwa pamoja changamoto za dunia na kudumisha amani na utulivu wa dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha