Viongozi wa China watoa salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa maofisa waandamizi wastaafu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 27, 2025

BEIJING - Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wametembelea au kuwapa majukumu wengine kutembelea maofisa waandamizi wastaafu ili kutoa salamu za sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, ambayo itaangukia Januari 29 mwaka huu.

Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), na viongozi wengine wamewatakia maofisa hao waandamizi wastaafu sikukuu njema ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, afya njema na maisha marefu.

Maofisa hao waandamizi wastaafu wamesifu sana kazi ya Kamati Kuu ya CPC katika mwaka uliopita na wameonyesha kuunga mkono kwa moyo wote nafasi kuu ya Xi kwenye Kamati Kuu ya CPC na katika Chama kwa ujumla.

Wameeleza matumaini yao kuwa Chama, wanajeshi na watu wa makabila yote ya China watashikamana kwa karibu zaidi na Kamati Kuu ya Chama ambayo Komredi Xi Jinping akiwa kiongozi wake mkuu, ili kuijenga China kuwa nchi yenye nguvu zaidi, kufuata njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa na kufikia ustawishaji mkubwa wa taifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha