

Lugha Nyingine
Visa Zasababisha ongezeko la Watalii wa Kigeni Wanaowasili China
Watalii wa kigeni wakisubiri ukaguzi wa kuingia China katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Pudong mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Januari 15, 2025. (Picha na Huang Bo/Xinhua)
BEIJING – Wakati ambapo China ikiendelea kulegeza sera zake za kusafiri nchini China bila visa, nchi hiyo imeshuhudia ongezeko kubwa la wasafiri kutoka nchi za nje, wakati wa kipindi cha pilika za wasafiri wengi cha Mwaka Mpya wa Jadi wa China, wakiwa na shauku ya kujionea na kufurahia utamaduni wenye mambo mengi za jadi wa China.
Kipindi cha wasafiri wengi cha Mwaka Mpya wa Jadi wa China, au “Chunyun” kwa lugha ya Kichina, lilianza Januari 14 na litaendelea hadi Februari 22. Takwimu za awali zinaonyesha kuwa oda za tiketi za ndege kwa abiria wanaoingia China kutoka nje katika kipindi hiki zimeongezeka kwa asilimia 47 kuliko mwaka jana wakati kama huo.
Msafiri kutoka Japan Kyoko Shimada alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Hongqiao, alikaribishwa na taa nyekundu za jadi na kazi za sanaa ya kukata karatasi zenye maandishi ya lugha ya Kichina "fu," ishara ya bahati nzuri.
Wakiwa walikuwa na ndoto ya muda mrefu kutembelea China, Shimada na mumewe wamechukua fursa hiyo ya kusafiri muda mfupi tu kabla ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, wakitumia fursa ya sera ya China ya kusamehe visa kwa raia wa Japan.
"Ingawa uwanja wa ndege ulikuwa na pilika nyingi kabla ya likizo, mchakato wa uhamiaji umekuwa mzuri na wa haraka kuliko nilivyotarajia. Maelekezo yalikuwa dhahiri, na mengine yalikuwa kwa lugha ya Kijapani," Shimada amesema.
Katika siku tatu mjini Shanghai, wanandoa hao wanapanga kutazama maonyesho ya taa ya kijadi katika Bustani ya kale ya Yuyuan na kuonja vyakula vya kienyeji mjini humo.
Mwaka 2024, China ililegeza zaidi sera zake za kusamehe viza kwa watu wa nchi za nje ili kuongeza ufunguaji mlango na kuhimiza mawasiliano kati ya watu na watu, ikiruhusu wasafiri na wafanyabiashara zaidi wa kigeni kutembelea nchi hiyo bila visa.
Jambo kubwa muhimu ni kuanzishwa kwa sera ya upande mmoja ya kusamehe visa mwezi Novemba 2024, ikiruhusu wamiliki wa pasipoti za kawaida kutoka nchi 38 kuingia na kukaa nchini China kwa hadi siku 30 bila visa.
Mwezi uliofuata, China ilitangaza kulegeza sera yake ya kusamehe visa kwa abiria wanaopita China kuunganisha ndege, ikiongeza muda unaoruhusiwa kukaa nchini humo kwa abiria hao wa kigeni hadi saa 240, kutoka kiwango cha awali cha saa 72 au 144.
Kwa mujibu wa tovuti ya mtandao ya Trip.com, ambayo ni kampuni kubwa ya huduma ya usafiri ya mtandaoni ya China, oda za wasafiri wanaoingia China kutoka kwa watalii wa kigeni ziliongezeka kwa asilimia 203 wakati wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kuliko mwaka jana, huku sehemu kubwa ya wageni hao wakitoka Korea Kusini, Malaysia, Singapore na Japan.
Watalii wa kigeni wakijaza fomu za kuingia China katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shanghai Pudong mjini Shanghai, Mashariki mwa China, Januari 15, 2025. (Picha na Huang Bo/Xinhua)
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma