

Lugha Nyingine
Mkuu wa Jeshi la Sudan asema vita dhidi ya vikosi vya wanamgambo vinakaribia kuisha
Picha hii iliyotolewa na Baraza la Mamlaka ya Mpito ya Sudan ikimuonyesha afisa wa jeshi la Sudan (kulia, mbele) akimkaribisha Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) Abdel Fattah Al-Burhan (kushoto, mbele) alipowasili katika mji wa Omdurman, kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum, Machi 12, 2024. (Xinhua)
KHARTOUM - Mwenyekiti wa Baraza la Mamlaka ya Mpito ya Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kwamba vita dhidi ya wanamgambo wa Vikosi vya Mwitikio wa Haraka (RSF) vinakaribia kuisha na kwamba uasi huo utatokomezwa.
Al-Burhan, ambaye pia ni kamanda wa Vikosi vya Jeshi la Sudan (SAF), ametoa kauli hiyo Jumapili alipokuwa akitembelea makao makuu ya Kamandi Kuu ya SAF katika mji mkuu Khartoum, ambayo hivi karibuni iliachiliwa huru kutoka kwenye hali ya kuzingirwa na RSF kwa miezi 21, taarifa iliyotolewa na baraza hilo imeeleza.
"Vita vinakaribia mwisho wake na uasi utatokomezwa. Ahadi yetu kwa watu wa Sudan ni kwamba tutapambana na wahalifu hawa hadi tuwashinde," Al-Burhan amewaambia wanajeshi.
"Vikosi vya kijeshi vina uwezo na uhimilivu. Havitashindwa, na historia yao inajieleza yenyewe," amesema.
Siku ya Ijumaa, jeshi hilo la Sudan lilitangaza kuwa limevunja mazingirwa ya Makao Makuu ya Kamandi Kuu yake, ambao umekuwepo tangu kuzuka kwa vita hivyo mwezi Aprili 2023.
Kamandi Kuu hiyo, iliyoko katikati mwa Khartoum, inajumuisha majengo makuu matano, yakiwemo Makao Makuu ya Jeshi, Kamandi ya Kikosi cha Majini, Makao Makuu ya Kikosi cha Anga, Idara ya Ujasusi ya Jeshi, na Wizara ya Ulinzi.
Sudan imekuwa katika mgogoro mbaya kati ya SAF na RSF tangu katikati ya Aprili 2023, ambao umesababisha vifo vya watu 28,000 na kufanya wengine zaidi ya milioni 15 kuwa wakimbizi, ama ndani au nje ya Sudan, kwa mujibu wa makadirio mapya ya mashirika ya kimataifa.
Picha hii iliyotolewa na Baraza la Mamlaka ya Mpito ya Sudan Agosti 24, 2024 ikimuonyesha Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF) Abdel Fattah Al-Burhan (kulia, katikati) karibu na Khartoum, Sudan. (Xinhua)
Shughuli mbalimbali za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China zafanyika katika Nchi Nyingi
Muonekano wa Kisiwa cha Weizhou katika Mkoa wa Guangxi, Kusini mwa China
Hafla ya Kukaribisha Panda wa China yafanyika katika Bustani ya Wanyama ya Adelaide, Australia
Shughuli mbalimbali zafanyika sehemu mbalimbali China kukaribisha Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa China
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma