Rais wa Zambia atuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa watu wa China

(CRI Online) Januari 31, 2025

Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi kwa watu wa China na kuzitakia nchi hizo mbili ustawi na mafanikio.

Rais Hichilema amesema, urafiki wa kina kati ya Zambia na China utachukua fursa ya Sikukuu hiyo kuendelea kuimarishwa.

Amesema katika kipindi cha Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China, anapenda kutoa salamu za dhati kwa watu wa China na kuzitakia nchi zote mbili mafanikio katika miaka ijayo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha