Rais wa DRC asema atafanya kila awezalo kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na wanajeshi wanaoipinga serikali

(CRI Online) Januari 31, 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Félix Tshisekedi amesema hali ya usalama mashariki mwa DRC inaendelea kuzorota na serikali yake itafanya kila iwezalo kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na kundi la waasi la M23.

Akizungumza katika hotuba yake kwa taifa kupitia televisheni ya nchi hiyo, Rais Tshisekedi amesema kundi la M23 limeongeza mashambulizi yake mjini Goma, mji mkuu wa Jimbo la Kivu Kaskazini, na maeneo mengine.

Amesema serikali yake imechukua hatua madhubuti kuongeza uungaji mkono wa kifedha kwa jeshi na kuimarisha ushirikiano na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ili kurejesha maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa kundi la M23.

Rais Tshisekedi ameongeza kuwa, licha ya operesheni za kijeshi, DRC itasisitiza kupatikana kwa amani ya kikanda haraka iwezekanavyo kupitia njia za kidiplomasia kama Azimio la Luanda.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha