Mkuu wa Zimamoto asema hakuna mtu anayetazamiwa kunusurika katika ajali ya kugongana kwa ndege iliyotokea nchini Marekani

(CRI Online) Februari 01, 2025

Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto na Huduma za Dharura za Matibabu katika Wilaya ya Columbia nchini Marekani, John Donnely, amesema huenda hakuna mtu aliyenusurika katika ajali ya ndege ya abiria na helikopta ya jeshi kugongana angani karibu na Uwanja wa Ndege wa Reagan jumatano wiki hii.

Donnely amesema, kwa sasa operesheni inabadilishwa kutoka uokoaji na kuwa ya kutafuta miili, na hana imani kama kuna watu walionusurika katika ajali hiyo.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa, wamepata miili 27 kutoka kwenye ndege na mwili mmoja kutoka kwenye helikopta ya jeshi.

Ndege ya American Airlines iliyokuwa na abiria 60 na wahudumu wanne iligongana na helikopta ya jeshi iliyokuwa na askari watatu usiku wa alhamis kwa saa za huko.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha