Mlipuko wa Ebola watokea tena nchini Uganda

(CRI Online) Februari 01, 2025

Wizara ya Afya ya Uganda imetangaza jana kwamba ugonjwa wa Ebola umeibuka tena nchini humo baada ya miaka miwili, ambapo muuguzi mmoja katika Hospitali ya Rufaa ya Mulago iliyoko Kampala, amefariki kutokana na ugonjwa huo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya nchini humo, Bibi Diana Atwine amesema, matokeo ya vipimo kutoka maabara yalionyesha kuwa muuguzi huyo aliambukizwa virusi vya Ebola vya Sudan na hadi sasa, watu 45 waliowasiliana naye kwa karibu, ikiwemo familia yake na wafanyakazi wa matibabu, wametengwa kwa uangalizi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa jana likisema, limetenga dola za Marekani milioni moja kutoka kwa fedha husika za dharura kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko huo, na linapanga kupeleka vifaa vya matibabu nchini Uganda.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha